Kutoa ni moyo na sio utajiri.....Wanafunzi chuo kikuu Iringa kumchangia mwenzao kutokana na juhudi alizo onyesha kwao
Wengi
waonyesha kuguswa juu ya uelekeo wa
mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa.
Wanafunzi wa kitivo cha sanaa ya sayansi na mahusiano
ya jamii hususani wale wa shahada ya Uandishi wa Habari na Utangazaji mwaka wa
tatu katika chuo kikuu cha Iringa
waonyesha kuguswa juu ya jitihada zilizofanywa na mmoja wa wanafunzi chuoni
hapo juu ya uelekeo wake kielimu alionao.
Mwanafunzi huyo ajulikanae kwa jina la Joel John Haule
ambaye ni mlemavu wa miguu hutegemea zaidi baiskeli ndogo kutembelea kwa msaada
wa kusukumwa anasoma stashahada
(Diploma) ya maendeleo ya jamii chuoni hapo kwa mwaka wa kwanza sasa amekua
akifanya vizuri sana darasani hivyo kupelekea wanafunzi wenzake kuweza kuguswa
na kujitolea kumchangia kiasi cha pesa ili kiweze kumsaidia katika matumizi
madogodogo chuoni hapo kutokana na kukosa msaada zaidi wa kifedha na mahitaji
mengine juu ya elimu yake.
Wanafunzi hao waliweza kuchanga kiasi cha Tsh.69,000/=
kwa ghafla muda waliokua darasani kuweza kumsaidia mwenzao huyo wazo
lililotolewa na mmoja wa wanafunzi wa uandishi wa habari Tumaini Msowoya wakiwa
katika mjadala uliotokana na somo lililokuwa likifundishwa na mwalimu Mr. Nduye
M. ambaye ndiye mwalimu wa somo la kanuni za ufundishaji (Principle of
Teaching).
Wazo hilo lilitiliwa mkazo na kufafanuliwa zaidi na
mwalimu huyo mpaka kupelekea wengi wa wanafunzi hao kujikuta wakiguswa kitendo
kilicho pelekea wao kuamua kumchangia mwanafunzi huyo.
Hata hivyo Joel aliweza kuwashukuru wanafunzi hao kwa
ukarimu walionao na kuweza kuonyesha hisia zao juu ya watu wenye ulemavu
kuwaona kuwa nao kumbe wanaweza katika elimu hususani elimu ya juu, pia aliweza
kutoa ushauri kwa watu wenye ulemavu kama yeye kuweza kujitangaza (expose) kwa
jamii juu ya ulemavu wao ili waweze pata misaada na mawazo mbali mbali ili
waweze kujichanganya na watu wengine ambao sio walemavu ili waweze kubadilika
na si kujitenga na kukaa kwa mawazo kutokana na hali waliyonayo.
Joel mpaka sasa anakabiliwa na tatizo la kifedha zaidi
kutokana na maumbile aliyonayo ya ulemavu wa miguu hivyo kumpelekea kuto
jiingiza katika shughuri za kuingiza kipato ili kuweze kumkidhi katika mahitaji
yake ya kimaisha .
Pia anahitaji msaada zaidi juu ya maisha aliyonayo
chuoni hapo katika mazingira ya ada ya chuo, chakula, mavazi pamoja na fedha za
steshonari ili kuweza kufanikisha malengo yake kwani anataraji kusoma na kuweza
kufika katika ngazi ya juu kielimu. Hivyo kwa wale wote waliotayari kujitolea waweza
tuma msaada wako kupitia namba yake ya simu ya mkononi ambayo ni 0769694831
(kwa njia ya M-Pesa).
0 comments:
Post a Comment