ZAWADI YA MEI MOSI KWA WANANCHI WOTE!!!! HUSUSANI WANA KYELA

Ujio wa Mei mosi kwa KPC ni mwangaza kwa wananchi wote Tanzania!!!

Uongozi wa chuo cha biashara na ufundi anuai cha Kyela Polytechnic College unafanya maandalizi makubwa juu ya kupokea siku kuu ya wafanyakazi ambayo huazimishwa kila mwaka mwezi wa tano tarehe mosi.

Ikiwa ni mara ya kwanza kwa chuo hicho kushiriki tangu kuanzishwa kwake uongozi umeweza kufafanua zaidi na kudai kuwa wameweza kujiandaa vizuri katika kila idara na kuweza kukamilika katika siku za mwanzo kabla ya siku husika ambapo kutakua na maonyesho ya huduma mbalimbali ambazo hutolewa na chuo hicho hivyo wameweza kuwasii watu kujitokeza kwa wingi siku za maonyesho na kuweza kutembelea banda la maonyesho la chuo hicho kwa wingi zaidi.

Akitoa ufafanuzi zaidi afisa masoko wa chuo hicho Ndg. Baraka Philipo alisema kuwa ingawa ni kwa mara ya kwanza twaingia katika maonyesho haya lakini tumeweza kujiandaa vilivyo juu ya ujio wa sikuu kuu hii ya wafanyakazi, hivyo naomba wana kyela na mbeya kwa ujumla wajitokeze kwa wingi kushuhudia baadhi ya vitu tutakavyo kua navyo wakati wa siku za maonyesho hayo nakujua hata baadhi ya kozi zinazotolewa na chuo chetu na taarifa nyingine muhimu.

Pia aliongeza kusema watatumia nafasi hiyo kutangaza baadhi ya taarifa muhimu za chuo hivyo ni vyema watu wakajiyokeza zaidi karibu na banda letu ili kuweza pata taarifa muhimu za chuo.

Siku kuu hiyo ya wafanyakazi itaadhimishwa kimkoa wilayani Kyela ambapo itaanza kuadhimishwa na maonyesho mbalimbali kuanzia tarehe 24 mwezi huu wa nne nakufanyika katika viwanja vya mwakangale(BOMANI) mpaka siku yenyewe ya mei mosi.

 Source: Maona LE(BAJ).

0 comments:

Post a Comment