WANANCHI (WADAU WA ELIMU) WILAYANI KYELA WAJITOKEZA KUJADILI JUU YA KUSHUKA KWA KIWANGO CHA ELIMU WILAYANI HUMO. 

Wadau wa elimu wilayani kyela wamewataka Wazazi na walezi kufuatilia maendeleo ya vijana wao mashuleni badala ya kuwaingiza katika biashara wakati wanaendelea na masomo kitu ambacho huathiri maendele ya kitaaluma kwa vijana hao.
Wakiongea katika mdahalo wa wadau wa elimu wilayani hapa uliolenga kujua nini chanzo cha kushuka kwa elimu wilayani hapa, Baadhi ya wadau wamewalalamikia wazazi kwa kutofuatilia maendeleo ya vijana wao shuleni hivyo kutokujua changamoto zinazowakabili waalimu juu ya tabia za vijana wao.
Meneja wa Maisha Ambangile ambaye ni miongoni mwa wadau walioandaa mdahalo huo amesikitishwa na tabia za baadhi ya wazazi willayani hapa kwa kuwahusisha vijana wao ambao ni wanafunzi kwenye biashara za bodaboda, kuchoma mishikaki na nyinginezo ambazo huchangia kushuka kwa elimu wilayani humo na kusabisha wilaya hiyo kubuluza mkia kitaaluma mkoani mbeya.
Wakati huo, mwenyekiti wa mdahalo huo Dr. Salatiel Mwakyambiki Ambae pia ni mkuu wa chuo cha KPC kilichopo wilayani hapa, amewataka wasomi wa wilaya hiyo kuwa mfano wa kuigwa na wasiosoma kwa kutumia fursa za taaluma waliyonayo badala ya kuungana na wasiosoma katika tabia zisizofaa faa hivyo kuifanya elimu kutokua na mvuto.
Nao wadau ambao kitaaluma ni walimu wameelezea changamoto zinazowakabili mashuleni wilayani hapa ikiwemo ushirikiano baina ya wazazi na walimu, wanafunzi na waalimu na kubadilishwa kwa mitaala kama changamoto inayosababisha kushuka kwa elimu wilayani hapa.
Mwalimu Grina Tirio, amesikitishwa na tabia ya wazazi kuwa wepesi kuchangia sherehe za harusi, 'vipeimara' na sherehe nyingine kuliko hata hela ya 'tuisheni' kwa vijana wao kitu ambacho hukatisha tamaa kwa walimu wenye moyo wa kujitolea wilayi hapa.
Akiongea katika mdahalo, Thobias Mwamkonda ambaye amewai kuwa mwenyekiti wa wanafunzi wa elimu ya juu watokao wilayani kyela amedai kuwa baadhi ya wazazi wilayani hapa hawana moyo wa dhati wa kujitolea kusomesha watoto wao hivyo kusababisha kiwango cha elimu kushuka wilayani huapa kwa siku za hivi karibuni.
Mdahalo huo ulilenga kutatua tatizo la kushuka kwa elimu wilayani hapa ikizingatiwa kuwa kyela kwa miaka ya karibuni imekuwa mkiani kitaaluma ukilinganisha na wilaya nyingine za mkoani mbeya

Baadhi ya wazee na wadau wa elimu wilayani kyela wakiwa katika mdahalo uliofanyika katika ukumbi wa KBC wakijadili juu ya kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani humo.

0 comments:

Post a Comment