26 Wauawa nchini Nigeria!!.
Watu 26 nchini Nigeria wauawa katika shambulio lililo fanywa na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la boko  Haram hili ikiwa ni shambulizi lililo tokea hivi karibuni wakati nchi hiyo ikiwa katika  kitendawili cha kuwatafuta na kuwaokoa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa na kundi nhilo nchini humo.

Shambulizi hilo lilifanyika katika kijiji kimoja kilichopo kaskazini mashariki mwa Nigeria karibu na eneo ambalo wasichana hao walitekwa mweai jana na kundi hilo la bokO  Haram.
Hata hivyo shambulio hilo limetokea baada ya milipuko miwili kutokea mjini jos katika jimbo la plateau lililo sababisha vifo vya watu takribani 118 jumanne usiku ikiwa mpaka sasa juhudi za kutafuta maiti hao zikiwa bado zinaendelea.
Chanzo cha habari kinasema kuwa shambulio hilo lililo fanyika mjini pia lilisababishwa na kundi hilo la waasi la kiisilamu la boko Haram.